MIMBA ZA MAPEMA

By July 13, 2020 July 27th, 2020 Voice

Likuwa nimetamauka

Mawazo linilemea

Sioni uhakika 

Wa masomo kuendelea 

Mimba zimechipuka

Furaha imevurugika

HUKO NJE KWA PAPASA 

MIMBA ZA MAPEMA ZISIWEPO

Likizo liwaidia

Muhula haukukamilika

Nyumbani mkaelekea

Shuleni mkaondoka

Rai nawapatia 

Msidhani ni dhihaka

HUKO NJE KWA PAPARA

MIMBA ZA MAPEMA ZISIWEPO

Mjikinge na wendani

Waso na mema maoni

Yote yalovitabuni

Uyatie akilini

Usimame na manani

Kila mara maombini

HUKO NJE KWA PAPASA

MIMBA ZA MAPEMA ZISIWEPO 

Magoha keshasema

Nakushauri mwanangu 

Watanunua ta soda

Wakunase mwanangu 

Nakukanya ewe sada

Sikiya maneno yangu 

HUKO NJE KWA PAPASA

MIMBA ZA MAPEMA ZISIWEPO

Sasa limekuwa shaka 

Mimba zimechipuka 

Machozi yanapuputika

Niwapi pamekoseka?

Serekali ina mikakati

Tena kwa uhakika

HUKO NJE KWA PAPASA MIMBA ZA MAPEMA ZISIWEPO

Tamati mi nifikile

Ujumbe mewasilimisha

Nawaomba wakwale

Elimu kuimarisha

Tuamke tusilale 

Masomo kuyadumisha

HUKO NJE KWA PAPASA 

MIMBA ZA MAPEMA ZISIWEPO.

By Asha Kabuka Mwamjimbo