Ni tunu ilo adhimu, mwana wa kiafurika
Ni tuzo ilo muhimu, hasa akielimika
Hilo tulilifahamu, ndiposa leo twawaka
Mwana wa kike hakika, leo asherehekewa
Haki anazomiliki, huru alizoachiwa
Ni nyingi zilo lukuki, wa kike alizopewa
Leo twapiga fataki, hini tunu tulopewa
Wakale walifinyanga, kumbe tuna wahandisi
Alinyimwa haki nyingi, zamani za madhalimuÂ
Haki zilo za msingi, wakike tulidhulumu
Kumbe ana tija nyingi, tena nyingi za muhimu
Afrika yametuka, wa kike katabasamu
Leo ingia ofisi, uone tavyopokewa
Mwanamke kiwa bosi, vyema utakirimiwa
Tena kwa wingi wa hisi, mazuri ukiyapewa
Kumbe ni tunu adhimu, wa kike wa afurika
Uongozi afahamu, kwayo yake moja nia
Kishika yake kalamu, kwa makini apangia
Atenda yalo muhimu, Leo tunafurahia
Wa kike tunu muhimu, sote tunajionea
Moyo wangu unacheka, nashindwa kuendelea
Haki ziliposemeka, bilaye kumuonea
Leo wameelimika, mazuri twajionea
Shangwe kwa wali wa kike, ni tunu ya Afrika
#Ashakabuka
#DadaRisingÂ
#DayoftheAfricanchild